Connect with us

Michuano ya soka, mzunguko wa mwisho kufuzu fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wasiodizi miaka 17 mwaka ujao nchini Madadscar zinachezwa mwishoni mwa wiki hii katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Hatua hii inakuja baada ya kumalizika kwa mzunguko wa pili wa michuano hii mwezi Agosti, ambapo vlabu 14 vilimenyana kufuzu katika hatua hii ya mwisho.

Mechi hizi zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi ataungana na wenyeji wa muchuano hiyo Madagascar katika fainali itakayopigwa mwezi Aprili mwaka ujao.

Ratiba ya michuano ya mwishoni mwa wiki:-

Ghana vs Ivory Coast

Niger vs Gabon

Mali vs Ethiopia

Senegal vs Guinea

Sudan vs Cameroon

Tanzania vs Congo

Angola vs Comoros

Michuano hii itachezwa nyumbani na ugenini.

More in