Connect with us

Na Victor Abuso,

Michuano ya kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN, itakayofanyika mwaka ujao nchini Kenya, inachezwa mwishoni mwa wiki hii.

Mzunguko wa kwanza

DRC vs Congo

Cameroon vs Sao Tome and Principe.

Leopard wako nyumbani baada ya wiki iliyopita, kutofungana na wapinzani wao katika mchuano muhimu uliochezwa katika uwanja wa Kintele, jijini Brazaville.

Mshindi kati ya timu hizi mbili atafuzu katika hatua hiyo.

Ukanda wa Afrika ya Kati unatoa timu tatu katika michuano hii, tayari Equitorial Guinea imefuzu kwa sababu Gabon ilijiondoa.

Cameroon ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-0 nayo ina nafasi nzuri kufuzu ikiwa itashinda mechi ya leo au hata kutoka sare.

Mzunguko wa pili

Nigeria vs Berlin

Cote d’ivoire vs Niger

Mali vs Mauritania

Nigeria wana kibarua kigumu, kuepuka aibu dhidi ya Benin ambayo iliifunga bao 1-0.

Super Eagles inahitaji kushinda mechi ya leo ili kujihakikishia nafasi ya kwenda Kenya kuwania ubingwa wa Afrika.

Ivory Coast nchi ambayo ina jina kubwa katika mchezo wa soka, ilianza vibaya dhidi ya Nigeria kwa kufungwa mabao 2-1 na leo wanahitaji ushindi ili kusonga mbele.

Kibarua kingine, ni kati ya Burkina Faso na Ghana, timu ambazo wiki iliyopita, zilitoka sare ya mabao 2-2.

Mzunguko wa tatu

Rwanda vs Uganda

Uganda ipo jijini Kigali kupambana na Rwanda baada ya kuishinda Rwanda mabao 3-0 wiki iliyopita.

Uwanja huu unachezwa katika katika uwanja wa Nyamirambo na Amavubi Stars wana kazi kubwa ya kuvuka mlima huo, ili kusonga mbele.

Mshindi atacheza na Uganda au Ethiopia.

Ratiba nyingine

Angola vs Madagascar

Zambia vs Afrika Kusini

Harambee Stars kuchuana na Msumbiji mechi muhimu ya kirafiki

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya, Harambee Stars Stanley Okumbi, amekitaja kikosi cha wachezaji 19 wa nyumbani wanaojiandaa kumenyana na Msumbiji katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki.

Mchuuano huo utapigwa tarehe 2 mwezi Septemba jijini Maputo.

Baada ya kipindi kirefu kukosekana katika kikosi cha Harambee Stars, mshambuliaji wa Gor Mahia George ‘Black Berry’ Odhiambo ni miongoni mwa wachezaji walioitwa.

Mbali na Odhiambo, mchezaji wa Nakumatt FC Kepha Aswani pia amejumuishwa katika hicho na wanaanza maandalizi jijini Nairobi.

Kocha Okumbi amesema amewaita wachezaji hao kutokana na uwezo wao walionesha katika michuano ya ligi kuu ya soka hivi karibuni.

Bernard Ochieng, anayechezea Vihiga United, Joe Waithera wa Wazito FC na Chris Ochieng kutoka Mathare United ni wachezaji wapya ambao wameitwa katika kikos cha taifa kwa mara ya kwanza.

Harambee Stars inajiandaa kwa fainali ya CHAN mwaka ujao lakini pia michuano ya mataifa bingwa barani Afrika dhidi ya Ghana na Ethiopia mwezi Machi mwaka ujao.

Kikosi kamili

Makipa: Boniface Oluoch (Gor Mahia), Patrick Matasi (Posta Rangers)

Mabeki: Benard Ochieng (Vihiga United), Harun Shakava (Gor Mahia), Musa Mohammed (Gor Mahia), Omar Mbongi (Ulinzi Stars), Simon Mbugua (Posta Rangers)

Viungo wa Kati: Ernest Wendo (Gor Mahia), Victor Majid (AFC Leopards), George Odhiambo (Gor Mahia), Jackson Macharia (Tusker), Daniel Waweru (Ulinzi Stars)

Washambuliaji: Samuel Onyango (Ulinzi Stars), Bonface Muchiri (Tusker), Kepha Aswani (Nakumatt), Masoud Juma (Kariobangi Sharks), Stephen Waruru (Ulinzi Stars), Joe Waithera (Wazito), Chris Ochieng (Mathare United)

More in