Connect with us

Michuano ya soka kutafuta bingwa wa makala ya 12 ya mashindano ya timu za taifa kwa upande wa wanawake barani Afrika, inafunguliwa Jumamosi katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde nchini Cameroon.

Wenyeji ambao wanashiriki katika michuano hii kwa mara 11, watafungua dimba dhidi ya Misri saa kumi na moja na nusu jioni saa za Afrika Mashariki.

Misri inashiriki katika michuano hii kwa mara ya pili, mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 1998, na kuondolewa katika hatua ya makundi.

Mataifa nane yanashiriki katika michuano hii na yamewekwa katika makundi mawili.

Kundi la A: Cameroon, Misri, Afrika Kusini na Zimbabwe

Kundi la B: Nigeria, Mali, Ghana na Kenya.

Siku ya Jumapili mabingwa watetezi Nigeria na ambao wameshinda taji hili mara tisa mwaka:- 1991,1995,1998,2000,2002,2004,2006,2010 na 2014, watafungua michuano hii dhidi ya Mali mjini Limbe.

Kenya ambayo inashiriki katika michuano hii kwa mara ya kwanza, itamenyana na Ghana ambayo imeshiriki katika michuano hii mara 11 na kumaliza katika nafasi ya pili mara tatu mwaka 1998, 2002 na 2006.

Ratiba ijayo kundi A Jumanne Novemba 22 2016

  • Cameroon vs Afrika Kusini
  • Zimbabwe vs Misri

Ratiba ijayo ya kundi B Jumatano Novemba 23 2016

  • Nigeria vs Ghana
  • Kenya vs Mali

More in AWCON