Tuangazie Kundi A
Misri
Inashiriki fainali za Kombe la dunia tangu ilipofanya hivyo mwaka 1990. Kwa ujumla imeshiriki kombe la dunia mara mbili, 1934 na 1990. Mara zote iliishia katika hatua ya makundi.
Kocha raia wa Argentina, Hector Cuper ambaye aliwahi kuzinoa Valencia ya Hispania na Inter Milan ya Italia atakiongoza kikosi hicho kaatikaa faainali za kombe la dunia, yaakiwa ni mafanikio makubwa kwake. Pia aliingoza Misri kufika fainali ya taji la Afrika mwaka 2017 dhidi ya Cameroon.
Goli la dakika ya 94 la Mohammed Salah katika mchezo wa mwisho dhidi ya Congo Brazaville ndilo lililoipeleka Misri kwenye fainali hizo.
Salah pia ndiye aliyefunga asilimia 71 ya mabao yote yaliyoiwezesha Misiri maarufu kama Faraos kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.
Essam El-Hadary, golikipaa wa Misri ana miaka 45 na endapo ataichezea Misri katika fainali hizo atavunja rekodi ya goikipa wa zamani wa Colombia Faryd Mondragon ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kushiriki fainali hizo. Mandraagon ambaaye aliichezea Colombia katika faainaali za mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 43.
Timu nyingine katika kundi hili.
Urusi
Urusi inashika nafasi ya 66 katika orodha ya viwango vya Fifa duniani. Imeshiriki fainali za Kombe la dunia mara 10 na mafanikio makubwa ni kufika hatua ya nusu fainali.
Kocha wake Stanslav Cherchesovni golikipa wa zamani wa kimataifa wa Urusi aliyeshiriki fainali za Kombe la dunia mwaka 1994 na za mwaka 2002. Alipewa jukumu la kuinoa Urusi mwaka 2016.
Urusi itamtegemea zaidi mshambuliaji Fedor Smolov
Igor Akinfeev ndiye mchezaji mzoefu, amecheza zaidi ya mechi 100 za timu ya taifa na ndiye nahodha wa Urusi.
Urusi itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Saudi Arabia Juni 14 katika Uwanja wa Luzhniki Mjini Moscow.
Saudi Arabia
Taifa hili la kiarabu limeshiriki fainali za Kombe la Dunia mara nne, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 1994
Juan Antonio Pizzi ndiye kocha wa timu hiyo, alichukua jukumu mwaka 2017 baaada ya kudumu kwa muda mfupi katika kikosi cha Chile ambaako alishindwa kuiwezesha timu hiyo kufuzu kucheza fainali za mwaka huu.
Mara ya mwisho Saudia ilishiriki fainali hizo mwaka 2002 zilipoandaliwa kwa pamoja na Korea Kusini na Japan.
Mohammed Al-Salhawi ndiye nyota tegemeo wa Saudi Arabia katika fainali hizo,pia alikuwa mfungaji bora katika mchakato wa kuwania tiketi ya kwenda Urusi ambapo aliifungia nchi yake mabao 16.
Uruguay
Imeshiriki fainali za Kombe la dunia mara mara 12 ikishinda taji hilo mara mbili, mwaka 1930 na 1950. Pia imefika hatua ya nusu fainali mara tano.
Kocha wa timu hiyo Oscar Tabarez ana historia kubwa na timu hiyo, chini yake imecheza fainali za kombe la dunia 1990, 2010 na 2014. Anasifika kwa mbinu mbalimbali ikiwemo ya ushambuliaji.
Luis Suarez na Edinson Cavani ndio washambuliaji tegemeo kwa timu hiyo katika fainali za mwaka huu.
#WCsoka25