-
-
by
Victor Abuso
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Mfaransa Sebastian Migne amesema, rais wa Shirikisho la soka nchini humo Nick Mwendwa anaweza kumfuta kazi iwapo anataka kufanya hivyo.
Migne ametoa kauli hii baada ya Kenya kuondolewa na Tanzania katika michuano ya kufuzu kucheza fainali ya CHAN Jumapili iliyopita, baada ya kufungwa mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penalti, jijini Nairobi.
Mechi hiyo ilifikia katika hatua hiyo, baada ya timu zote kutofungana katika muda wa kawaida, katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani.
“Iwapo Shirikisho linataka kujifta kazi, liendelee kufanya hivyo, lakini nina mashaka iwapo linaweza kunilipa iwapo litavunja mkataba wangu,” alisema.
“Iwapo wanapata wakati mgumu kulipa mshahara wangu, je wataweza kutekeleza matakwa ya wangu ?,” aliuliza.
Uongozi wa soka nchini Kenya, haujajitokeza kuzungumzia hatima ya kocha huyo kuendelea kuifunza Harambee Stars.
Migne alisaini mkataba wa miaka mitatu mwaka 2018, kuifunza Harambee Stars na baada ya AFCON mwaka 2019, ana kazi ya kuisaidia nchi hiyo kufuzu katika michuano ya 2021 na ile ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...