-
by
Victor Abuso
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars Charles Mkwasa anasema wachezaji wake wako tayari kuikabili Nigeria katika mchuano wa mwishoni mwa wiki hii kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Tanzania itakuwa mwenyeji wa Nigeria siku ya Jumamosi katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Vijana wa Taifa Stars kwa muda wa wiki moja iliyopita wamekuwa wakipiga kambi nchini Uturuki na walicheza mchuano wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Libya na kufungwa mabao 2 kwa 1.
Kocha Mkwasa ameiambia tovuti ya Shirikisho la soka TFF kuwa kambi hiyo imewasaidia vijana wake kujiamini na sasa wako tayari kumenyana na mabingwa hao wa zamani wa soka barani Afrika.
Aidha, amesifia mazingira ya kambi yao nchini Uturuki na kusisitiza imewapa mazingira ya kujiimarisha zaidi na wanakamilisha kambi yao siku ya Jumatatu kabla ya kurejea nyumbani kuisubiri Nigeria.
Tanzania ipo katika kundi moja na Misri pamoja na Chad.
Mchuano wa kwanza wa makundi Tanzania wakicheza wakiwa ugenini walifungwa na Misri mabao 3 kwa 0.
Kibarua cha Jumamosi kitakuwa kipimo cha Mkwasa ambaye alichukua mikoba ya Mart Nooij kutoka Uholanzi aliyefutwa kazi mwezi Juni.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...