Morocco imewasilisha rasmi ombi la kutaka kuwa mwenyeji wa kombe la dunia katika mchezo wa soka mwaka 2026.
Siku ya Jumamosi, nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika, itazindua rasmi kampeni ya kutafuta uugwaji mkono.
Morroco imesema ikipata nafasi hiyo, itafanyika katika miji yake 12.
Aidha, inapanga kujenga viwanja vipya sita.
Inapambana na Marekani, Canada na Mexico.
Morocco imewahi kujairbu kuomba nafasi hiyo mwaka 1994, 1998, 2006 na 2010 bila mafanikio.
Ikifanikiwa, itakuwa nchi ya pili ya Afrika kuandaa fainali hiyo baada ya Afrika Kusini mwaka 2010.
Hatima ya Morocco itafahamika mwezi Juni, wakati wa Mkutano Mkuu wa FIFA utakaofanyika jijini Moscow nchini Urusi.