Na mwandishi wetu akiwa Dar es Salaam,
Leo kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) inayoongozwa na mwenyekiti wake Elias Mwanjala imefikia tamati na kutoa hukumu kuhusiana na mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Bernard Morrison.
Mchezaji Morrison na iliyokuwa klabu yake walifikishana katika kamati hiyo kwa Morrison kudai kuwa yeye ni mchezaji huru hana mkataba na Yanga kwani mkataba wake wa miezi sita ulishamalizika huku Yanga wao wakidai walimuongeza mkataba wa miaka miwili.
Kamati hiyo imeeleza kuwa mkataba wa Yanga na Morrison unaodaiwa kuwa wa miaka miwili una mapungufu wakati hivyo Morrison anashinda ila wanampeleka katika kamati ya maadili sababu ameonesha dharau katika kamati hiyo baada ya kusaini mkataba na Simba shauri lake likiwa bado limaendelea.
“Picha haitoshi kuonesha kwamba mkataba ulisainiwa japo Morrison anaeleza kuwa siku ile alikwenda lakini hakusaini, maneno matupi hawezi kusaidia mkataba unaonesha ulisaini tarehe 20 March lakini wenyewe juu una.