Na Fadhili Sizya
Mtanzania Farid Mussa leo hii usiku anaweza akaandika historia mpya ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu ya soka nchini Hispania(La Liga) ambapo klabu yake CD Tenerife itacheza mchezo wa pili wa mtoano kutinga katika ligi hiyo dhidi ya Getafe.
Mechi hiyo itaanza saa 4:00 Usiku katika uwanja wa nyumbani wa Getafe Coliseum Alfonso Pérez.
Aidha mechi ya awali Tenerife walishinda bao 1-0 lililofungwa na Jorge Saenz uliochezwa kwenye uwanja wa Heliodoro Rodriguez Lopez.
Farid Mussa alijiunga na Tenerife akitokea Azam FC mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufuzu majaribio yake ya wiki mbili ambapo msimu wote uliopita alikuwa akitumika kikosi cha pili cha klabu hiyo.