Connect with us

Muianga ateuliwa kocha mpya wa Msumbiji

Muianga ateuliwa kocha mpya wa Msumbiji

Na Victor Abuso,

Beki wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Msumbiji Helder ‘Mano Mano’ Muianga amechukua mikoba ya Joao Chissano kuwa kocha wa timu ya taifa “The Mambas”.

Kibarua cha Chissano kiliota nyasi baada ya kufungwa na Rwanda bao 1 kwa 0 katika mchuano wa kwanza wa kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Muianga alikuwa msaidizi wa Chissano katika mchuano huo wa mwishoni mwa juma lililopita jijini Maputo.

Kabla ya mchuano dhidi ya Rwanda, Chissano aliiongoza Msumbiji hadi katika fainali ya michuano ya Kusini mwa Afrika COSAFA mwisho uliopita na kufungwa na Namibia.

Chissano anakuwa kocha wa pili barani Afrika kufutwa kazi baada ya Young Chimodzi wa Malawi.

Kazi kubwa ya kocha mpya Muianga, ni kukiandaa kikosi cha wachezaji wanaocheza nyumbani katika michuano ya kufuzu katika mechi za CHAN dhidi ya Ushelisheli mwishoni mwa juma hili mjini Beira.

Muianga alipokuwa mchezaji licha ya kuichezea Msumbuji, aliwahi pia kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini na Hungary.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in