Rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bility amefanikiwa kuwasilisha ombi la kuwania urais wa Shirikisho la soka duniani FIFA.
Bitily, mwenye umri wa miaka 48 alimtuma Meneja wake Edwin Snowe ambaye alikutana na Kaimu Katibu Mkuu wa FIFA Marcus Kattne jijini Zurich nchini Uswizi.
FIFA inasema, Bitly amekubaliwa kwa sababu amepata uungwaji mkono kutoka kwa Mashirikisho matano ya soka barani Afrika kama inavyotakiwa.
Hadi sasa Bility anakuwa mwafrika wa pili kuwahi kuonesha nia na kuwania wadhifa huo baada ya Issa Hayatou kuwania mwaka 2002 bila mafanikio.
“Ikiwa tunataka kubadilisha mchezo wa soka, ni lazima tuhakikishe kuwa wale waliokuwa ndani ya Shirikisho kati ya miaka 20 na zaidi hawahusiki tena,” alisema Bility.
Musa Bility anaugana na Mwanamfalme wa Jordan Ali Bin al-Hussein, mchezaji wa zamani wa Trinidad and Tobago David Nakhid, Jerome Champagne aliyekuwa wakati mmoja Naibu Katibu Mkuu wa FIFA Jerome Champagne na rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini.
Yeyote anayetaka kuwania urais wa FIFA ana hadi siku ya Jumatatu usiku kuwasilisha maombi yao.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyka tarehe 26 mwezi Februari mwaka ujao.