-
by
Victor Abuso
Mutasim Jaffer kutoka nchini Sudan amechaguliwa rais mpya wa Shirikisho la soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.
Jaffer ataongoza Shirikisho hilo kwa muda wa miaka minne ijayo na anachukua nafasi ya Leodegar Tenga kutoka Tanzania ambaye amekuwa katika wadhifa huo kwa miaka minane iliyopita.
Rais huyo mpya wa CECAFA alipata kura 6 kati ya 10 zilizopigwa huku mpinzani wake wa karibu Lawrence Mulindwa kutoka nchini Uganda akipata kura tatu na Vincent Nzamwita akipata kura moja.
Rais wa zamani Tenga amesema ana imani na matumaini makubwa kuwa rais huyo mpya atasaidia kuinua soka katika Ukanda huo.
“Nina furaha kubwa ya kukabidhi madaraka kwa mtu ambaye najua ana mapenzi makubwa na ya dhati katika mchezo wa soka.Tungependa kuiona CECAFA ikikua hatua kwa hatua,”.
“ Nina furaha kuwa nimefanya bidii nilivyoweza kwa kipindi chote cha miaka minane niliyokuwa rais wa CECAFA na nitafanya majukumu yoyote nitakayopewa katika siku zijazo,” alisema Tenga.
Rais huyo mpya wa CECAFA amesema atatumia uzoefu wake nchini Sudan kujaribu kuinua soka Afrika Mashariki na Kati.
Aidha, ameonesha kutoridhishwa na mataifa kutoka ukanda wa CECAFA kutofanya vizuri katika mashindano ya kufuzu katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Uchaguzi huu umefanyika siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya soka ya CECAFA mwaka 2015 jijini Addis Ababa.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...