Fainali ya pili kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, itachezwa siku ya Jumamosi kati ya Wydad Casablabca ya Morocco na Al-Ahly ya Misri.
Mchuano huu unakuja wiki moja baada ya timu zote mbili kutoka sare ya bao 1-1 mjini Alexandria katika fainali ya kwanza.
Al Ahly ambao wameshinda taji hili mara nane, watakuwa na kibarua kizito baada ya kukubali Wydad Casablanca, kupata bao la ugenini.
Klabu hii ya Misri imeshinda taji hili mwaka 1982, 1987, 2001, 2005, 2006, 2008, 2012, 2013.
Wydad Casablanca nayo ilishinda taji hili mara moja tu mwaka 1992.
Mshindi atapata kombe la kitita cha Dola za Marekani Milioni Mbili na Laki tano.
Timu hizi mbili, zilikutana katika hatua ya makundi na Wydad Casablanca kuongoza kundi hilo kwa alama 12 na Al Ahly kumaliza nafasi ya pili kwa alama 11.
Katika hatua hii, Wydad Casablanca ilishinda mechi nne, huku Al-Ahly ikishinda mechi tatu.
Historia ya timu zote mbili:-
Mwaka 2011
Ahly 3 Wydad 3
Wydad 1 Ahly 1
Mwaka 2016
Ahly 0 Wydad 0
Wydad 0 Ahly 1
Mwaka 2017
Ahly 2 Wydad 0
Wydad 2 Ahly 0
Fainali ya kwanza:-
Ahly 1 Wydad 1
Fainali ya pili:-
Wydad-Ahly