Kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Said Hamis Ndemla amefuyzu kucheza soka la kulipwa barani Ulaya katika klabu ya Elskistuna ya sweden.
Mchezaji huyo aliyechipukia katika timu ya vijana ya Simba kabla ya kupandishwa kwenye kikosi cha kwanza amefanya majaribio nchini Sweden kwa muda wa wiki mbili zilizopita.
“Amefanikiwa na baada ya hatua hii sasa tunasubiri kukaa chini na wenzetu kutoka Sweden ili tukamilishe mpango wa kumuuza Ndemla,”amesema manara akizungumza na mtandao huu wa soka25east.
Aidha Manara amesema Simba inaamini itaafikiana na Elskistuna ya Sweden kwakuwa lengo la klabu hiyo ni kuona wachezaji wanapata fursa kucheza soka nchini ya Tanzania kwa manufaa ya soka la taifa.
Ndemla anasifika kwa ubora katika eneo la kiungo hasa kwa uhodari wake wa kufunga mabao kwa mashuti ya mbali.
Tangu mwaka 2015 amekuwa akijumishwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa Taifa Stars na kufanikiwa kwake kutaongeza idadi ya wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje akiwemo Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars