Nigeria ilitoka sare ya bao 1-1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchuano wa Kimataifa wa kirafiki uliochezwa siku ya Jumatatu katika uwanja wa Adokiye Amiesimaka mjini Port Harcourt.
Super Eagles ilikuwa ya kwanza kupata bao, kupitia beki William Troost-Ekong baada ya kupata pasi murua kutoka kwa mshambualiaji Ogenyi Onazi.
Hata hivyo, DRC ilionekana kutawala muda mwingi wa mchezo huo, lakini ilipotimia katika dakika ya 78, Issam Mpeko aliisawazishia Leopard kupitia mkwaju wa penalti baada ya beki Ola Aina kufanya madhambi karibu na eneo la hatari.
Nigeria ilitumia mechi hiyo kama maandalizi ya michuano ya kombe la dunia, itakayoanza tarehe 14 mwezi Juni nchini Urusi.
Super Eagles imepangwa katika kundi la C na Argentina, Croatia na Iceland.
Kikosi hicho kinaondoka siku ya Jumanne kwenda Uingereza, kwa maandalizi zaidi na inatarjiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki tarehe 2 mwezi Juni.
Matokeo mengine ya michuano ya kirafiki yaliyochezwa Jumanne usiku:-
Kenya 1-0 Equitorial Guinea
Ureno 2-2 Tunisia
Ufaransa 2-0 Ireland
Korea 2-0 Honduras
Uturuki 2-1 Iran