Connect with us

Rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Sam Nyamweya amekanusha madai ya kufuja fedha za Shirikisho hilo wakati alipokuwa uongozini kabla ya kuondolewa kwake mapema mwaka 2016.

Uongozi wa FKF, unamtuhumu Nyaweya kwa kuchukua Dola za Marekani 25,000 kutoka katika akaunti ya fedha ya Shirikisho hilo.

Nyamweya amesema hajawahi kufuja fedha hizo zilizokuwa zimepangiwa kuimarisha soka vijijini katika eneo la Aberderes.

Pamoja na madai hayo, Halmashauri ya FKF imempata na kosa lingine la  kulishtaki Shirikisho hilo katika Mahakama za kawaida nchini Kenya kinyume na utaratibu wa FIFA zinataka kesi yoyote ya michezo kwenda katika Mahakama maalum ya Michezo.

FKF inasema baada ya kubaini Nyamweya alihusika katika makosa hayo amefungiwa kushiriki katika maswala ya soka nchini humo kwa miaka 10.

Nyamweya amesema uamuzi huo umemshangaza na kuongeza kuwa , hana cha kupoteza kwa sababu alishastaafu kuongoza soka na haiwezi akatumikia marufuku hayo.

Hata hivyo, amesema atakwenda Mahakamani kumshatki rais wa FKF Nick Mwendwa kwa kumharibia jina.

More in