Connect with us

 

Kocha wa Timu ya taifa ya soka ya Kenya Stanley Okumbi amewaita wachezaji watatu wanaocheza soka nchini Zambia kushiriki katika michuano miwili ya Kimataifa ya kirafiki dhidi ya Uganda na DRC wiki hii.

Wachezaji hao wanaochezea soka katika klabu ya Zesco United ni Jesse Were, David Owino na Anthony Okumu.

Watatu hao ni miongoni kwa wachezaji tisa wanaocheza soka nje ya nchi walioitwa na kocha Okumbi kuja kucheza katika michuano hii muhimu.

Harambee Stars itamenyana na Uganda Cranes siku ya Alhamisi na baadaye DR Congo siku ya Jumapili.

Mechi zote mbili zitachezwa katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos Mashariki mwa nchi hiyo.

Mataifa haya yanatumia michuano hii kujiandaa kwa michuano ya kufuzu kucheza kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2019 itakayoanza mwezi Juni.

Pamoja na hilo, Uganda na DRC zinatumia michuano hii kujiandaa kwa mechi za kufuzu kucheza fainali ya CHAN itakayofanyika mwaka 2018 nchini Kenya.

More in