Na Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema bado timu yake inakabiliwa na kibarua katika safu ya ushambuliaji.
Simba licha ya kuwafunga wapinzani wao Yanga katika mchezo wa ngao ya jamii jana katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo washambuliaji wake Laudit Mavugo na Emanuel Okwi walishindwa kuipasua ngome ya Yanga.
Omog raia wa Cameroon alisema atatumia siku zilizobaki kabla ya kucheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu.
“Ni changamoto , tunatengeneza nafasi lakini hatuzitumii. Ninarudi kuzungumza na vijana wangu,”alisema Omog aliyewahi kushinda Ligi ya Tanzania Bara akiwa na kikosi cha Azam FC.
Simba iliyotumia zaidi ya bilioni 1.3 za Tanzania kusajili wachezaji wapya na kuongeza mikataba ya wachezaji waliomaliza mkataba wake, itaanza kampeni ya kusaka taji la Ligi Kuu Jumamosi kwa kucheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Taifa