Timu ya taifa ya soka ya Ubelgiji inaorodheshwa ya kwanza na bora duniani kwa mujibu wa Shirikisho la soka duniania FIFA.
Hii ni orodha ya kwanza ya mwezi Januari mwaka huu wa 2016.
Argentina ni ya pili huku Uhispania ikiorodheshwa ya tatu.
Sweden imepanda nafasi moja na sasa ni ya 34, Iran ya 43.
Barani Afrika, Guinea imepanda nafasi moja na sasa inashikilia nafasi ya 49 duniani na ya saba barani Afrika.
Uganda pia imepanda nafasi moja na sasa inashikilia nafasi ya 62 duniani na ya 11 barani Afrika.
Cote d’ivoire bado inaongoza kuwa timu bora barani Afrika, Algeria inashikilia nafasi ya pili, Ghana ni ya tatu, Cape Verde ya nne na Tunisia ya Tano.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni ya kwanza, inashikilia nafasi ya 60 duniani na 10 barani Afrika.
Uganda ni ya pili katika ukanda huo, Rwanda ni ya pili na ya 22 barani Afrika huku ikiwa ya 91 duniani.
Kenya ni ya tatu na ya 25 barani Afrika na duniani inashikilia nafasi ya 101.
Burundi ni ya nne na ya 32 barani Afrika na duniani inashikilia nafasi ya 110 ikifuatwa na Ethiopia ambayo ni ya Tanzania ambayo ni ya 36 barani Afrika na ya 118 duniani.
Tanzania ni ya sita, inashikilia nafasi ya 38 barani Afrika na ya 126 duniani.
Djibouti, Eritrea na Somalia zinashikilia nafasi ya mwisho barani Afrika.