Connect with us

Rais wa Cameroon Paul Biya amesisitiza kuwa nchi yake iko tayari kuwa mwenyeji wa mashindano ya mataifa ya bara Afrika AFCON, yatakayofanyika mwaka 2019.

Hakikisho hili, limekuja baada ya rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad kukutana na rais Biya siku ya Jumanne jijini Yaounde.

Ahmad naye amesema kuwa, CAF haina mpango wa kuondoa mashindano hayo nchini Cameroon.

Rais Biya ametuhakikishia kuwa, atahakikisha kuwa maandalizi yote yanafanyika na kumalizika kwa wakati,” amesema Ahmad.

Cameroon ndio inayoandaa mashindano ya AFCON, sio CAF, kwa hivyo ni wao wa kutuambia kama wako tayari au la,” ameongeza.

Rais huyo wa CAF amesisitiza kuwa kukutana kwake na rais Biya, kulilenga kundoa wasiwasi kuhusu madai ya mashindano hayo kuondolewa nchini Cameroon.

Licha ya hakikisho hili, kumeendelea kushuhudiwa wasiwasi wa usalama hasa Kaskazini Magharibi mwa hiyo lakini pia ukarabati wa viwanja kufanyika taratibu.

Mashindano ya mwaka ujao kwa mara ya kwanza, yatajumuisha nchi 24, kutafuta mshindi katika michuano hiyo mikubwa itakayochezwa kati ya mwezi Juni na Julai.

More in