Shirikisho la soka duniani FIFA, limethibitisha kukamatwa kwa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad ambaye alikuwa amehudhuria mkutano mkuu wa FIFA, jijini Paris Ufaranasa.
Taarifa ya FIFA imesema Ahmad raia wa Madagascar, alikamatwa na kuhojiwa kuhusu madai mbalimbali kama rais wa CAF.
Hata hivyo, FIFA imesema kwa sasa haiwezi kutoa maelezo zaidi kuhusu kilichosababisha makamu huyo wa rais wa shirikisho hilo la soka duniani kutiwa mbaroni.
FIFA pia imewaomba maafisa wa uchunguzi nchini Uaransa kuwapa taarifa zozote walizonazo, zinazoweza kuwasaidia katika Kamati yake ya ambazo zinaweza kuziisaidia katika Kamati yake ya maadili.
Ahmad alichaguliwa kuwa rais wa CAF mwaka 2017 baada ya kumshinda rais wa zamani Issa Hayatou raia wa Cameroon aliyekuwa ameongoza soka barani Afrika tangu mwaka 1988.