Connect with us

Sababu zinazoangusha soka Afrika Mashariki na Kati

Sababu zinazoangusha soka Afrika Mashariki na Kati

Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati Kenya, Tanzania, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Eritrea, Sudan na Eritrea kwa mara nyingine wameshindwa kusonga mbele katika michuano ya kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza katika fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Matumaini yamesalia kwa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambazo zimefuzu katika hatua ya makundi lakini swali ni je, zitafanikiwa kuwa miongoni mwa mataifa matano yatakayoliwakilisha bara la Afrika ?

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewahi kufuzu katka fainali hizo mara moja tu katika historia ya soka mwaka 1974 wakati michuano hiyo ilipoandaliwa nchini Ujerumani.

Uganda haijawahi kufuzu na inaweka matumaini yake hai.Je itawezekana ?

Swali ambalo mashabiki wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati wanaendelea kuuliza ni kwanini mataifa hayo hayafiki mbalimbali katika soka la Kimataifa.

Sababu mbalimbali zimekuwa zikitolewa kwa muda mrefu sasa lakini cha ajabu ni kwamba suluhu haijapatikana.

Miongoni mwa sababu hizo ni pamoja na:-

1.Uongozi

Uongozi mbaya umeelezwa kuwa sababu kubwa inayosababisha mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kutofanya vizuri katika michuano hii. Mara nyingi viongozi wa soka wameelezwa kuwa na maslahi binafsi pindi wanapopata uongozi.

Hawajali maslahi ya wachezaji na yale ya wapenzi wa soka katika nchi yao. Swali ambalo limeendelea kuulizwa je, kiongozi wa Shirikisho la soka awe ni mtu aliyewahi kucheza soka ? Suala hili linaendelea kuzua tofauti za mara kwa mara.

2.Siasa

Soka katika mataifa mengi barani Afrika hasa Afrika Mashariki na Kati imeingizwa siasa chafu ikiwa na maana isiyokuwa na maendeleo. Mara nyingi tumewaona watu wanaotaka kuwania ubunge au udiwani katika nchi zao wakiwania uongozi wa soka ili kujipatia umaarufu na wanapopata wadhofa huo wanaachana na soka au kutotumia nafasi yao kusaidia kuinua soka.

3 Ufisadi

Fedha zinazotolewa na Shirikisho la soka duniani FIFA kwa lengo la kuimarisha soka katika mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa muda mrefu, zimekuwa hazitumiwi ipasavyo kuinua mchezo huo.

Mara nyingi tumesikia kupotea kwa fedha, wachezaji kutolipwa mshahara au wakati mwingine, Shirikisho la soka kutokuwa na uwezo wa kuwasafirisha wachezaji kwenda kucheza michuano muhimu na kuilazimu serikali kuingilia kati.

Mfano Kenya kabla ya kwenda Cape Verde, wachezaji waligoma kupanda ndege baada ya kulalamikia kutolipwa marupurupu yao lakini pia wakalazimika kusubiri saa nane, kabla ya kupanda ndege baada ya nauli ya wachezaji wote kutolipwa na kuilazimu seriklai kuingilia kati.

4. Maandalizi mabaya

Mara nyingi maandalizi ya michuano ya Kimataifa hufanyika kwa muda wa wiki moja ya mbili kabla ya mchuano wenyewe.Muda huu umekuwa mfupi sana kwa wachezaji kujiandaa vya kutsoha lakini pia kufahamiana vema kabla ya siku ya mchuano husika.Kutofahamiana vema kwa wachezaji kumesababisha mchanganyiko na kusabisha wachezaji kukosa utulivu au hata kugombania mpira.

5. Ligi kuu

Kiwango cha soka katika ligi kuu husika pia ni sababu ya kutofanya vizuri kwa sababu wachezaji wengi wa timu ya taifa wanatokea katika vlabu vinavyoshriki ligi kuu. Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati una wachezaji wachache sana wanaocheza soka Ulaya ukimwondoa Victor Wanyama kutoka nchini Kenya anayechgezea Southmptom ya Uingereza na wengine wachache.Mara nyingi ushindani katika ligi za mataifa hayo ni kati ya vlabu viwili au vitatu mfano Yanga, Simba na Azam vlabu ambavyomara nyingi zimeendelea kutoa wachezaji wa timu ya taifa.

6. Nidhamu

Baadhi ya wachezaji hawana nidhamu ndani na nje ya uwanja. Kuna wachezaji ambao wanakunywa pombe, kuvuta sigara au hata bangi saa kadhaa kabla ya mechi muhimu au hata kurushiana maneno makali kati yao wenyewe au na refarii.Hili ni tatizo ambalo linaathiri hali ya uchezaji.

7. Uzalendo.

Mashabiki wengi wa soka wameshakata tamaa na kukosa uzalendo kutokana na kushindwa kwa timu zao za taifa mara kwa mara, na kuanza kuzishabikia timu za Ulaya. Hata wachezaji wamejipata katika hili, wale wanocheza siku hizi hawajitoi kama wale wa zamani waliokuwa wanacheza ili kuinua jina la nchi yao, siku hizi soka imekuwa kama kazi kama sio biashara sio mbaya lakini imepunguza uzalendo.Huu ndio ukweli.

8. Soka la vijana

Mataifa yanayofanya vizuri katika soka la kimataifa kama Nigeria, Cameroon, Ghana, Ivory Coast na Algeria yana vikosi vya wachezaji chipukizi. Mataifa haya yana mashindano baina ya vijana na kuna taasisi maalum za kukuza vipaji hivyo.Hili limeonekana kushindikana katika mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.

Hizi ni baadhi tu za sababu zinazosababisha Ukanda wa Afrika Mashariki na Katu au CECAFA kufuzu kucheza kombe la dunia au lile la Afrika kwa muda mrefu sasa.

 

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in