Connect with us

Kundi H:

Kundi hili, lina Poland, Senegal, Colombia na Japan.

Mchuano wa kwanza wa kundi hili utakuwa kati ya Poland na Colombia tarehe 24 mwezi Juni, katika uwanja wa Kazan.

Ni kundi ambalo lina ushindani mkubwa.

Poland

Timu ya taifa ya PolandFIFA.COM

Imewahi kufuzu na kucheza katika fainai hii mara saba.

Mara ya kwanza kucheza katika fainali hii ilikuwa ni mwaka 1938. Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2006.

Mwaka 1974 na 1982, ilimaliza katika nafasi ya tatu.

Kocha wa timu hii ni Adam Nawalka tangu mwaka 2013. Aliwahi kuichezea Poland katika kombe la dunia mwaka 1978.

Mwaka 2006, aliwahi pia kuifikisha timu yake katka kombe la dunia.

Mchezaji wa kuangaliwa sana katika kikosi hiki ni nahodha Robert Lewandowski.

Aliongoza katika ufungaji wa mabao katika michuano ya kufika katika fainali hii kwa kuipa mabao 16.

Senegal

Timu ya taifa ya SenegalFIFA.COM

Ni mwakilishi mwingine wa bara la Afrika.

Imewahi kufuzu katika kombe la dunia mara moja tu mwaka 2002, mwaka huo ikifika katika hatua ya robo fainali.

Kocha wa timu hii ni Aliou Cisse, raia wa Senegal tangu mwaka 2015.

Alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofika katika hatua ya robo fainali mwaka 2002.

Mchezaji wa kuangaliwa sana katika kikosi cha Senegal ni Sadio Mane.

Uwezo wake mkubwa wa kukimbia na kufunga mabao unaelezwa kuwa utaisaidia timu hii katika michuano hii.

Umaarufu wake ulikuja baada ya kuhamia klabu ya Liverpool kwa Pauni Milioni 34 mwaka 2016.

Colombia

Timu ya taifa ya ColombiaFIFA.COM

Imewahi kufuzu katika michuano ya kombe la dunia mara tano.

Mara ya kwanza, ilikuwa ni mwaka 1962. Mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 2014.

Matokeo mazuri ya timu hii, ilikuwa ni mwaka 2014, ilipofika katika hatua ya robo fainali.

Kocha wa timu hii ni Jose Pekerman, tangu mwaka 2012.

Amewahi kuifikisha nchi yake katika kombe la dunia mwaka 2006.

Mchezaji maarufu ana anayeangaliwa sana katika kikosi hiki ni James Rodriguez, ambaye wakati wa kombe la dunia nchini Barzil mwaka 2014, alikuwa mfungaji bora.

Japan

Timu ya taifa ya Japan, imewahi kucheza katika fainali hii ya kombe la dunia mwaka tano.

Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 1998 huku mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2014 nchini Brazil.

Matokeo bora ilikuwa ni kwa Japan kufika katika hatua ya 16 mwaka 2002 na 2010.

Kocha wa Japan ni Akira Nishino, mchezaji wa zamani wa timu hii ya taifa.

Itakuwa mara yake ya kwanza kuipeleka Japan katika michuano ya kombe la dunia, licha ya mwaka 1996 kuisaidia timu yake kufika katika michuano ya Olimpiki na 1998 katika michuano ya dunia baina ya vlabu.

Mchezaji wa kuangaliwa sana katika timu hii ni Maya Yoshindna anayechezea klabu ya Southampton nchini Uingereza.

Amekuwa mchezaji muhimu wa timu hii tangu kombe la dunia mwaka 2012.

Ripoti ya Victor Abuso

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in