Klabu ya Simba SC kesho inatarajia kuandika historia kwa kumtangaza mwanahisa atakayemilikishwa asilimia 50 ya hisa za klabu hiyo maarufu nchini Tanzania.
Wanachama wa klabu hiyo watakutana jijini Dar es Salaam ambapo ili kumalisha mchakato ulioanza tangu mwaka jana wa kubadili mfumo wa uendeshaji kutoka ule wa kutegemea wanachama na kuwa wa hisa.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Haji Maanara amesema mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa wziri wa habari utamaduni, sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe.
“Tunakwenda kuandika historia kesho, mimi mwenyeqwe simmjui nani kashinda zabuni hii lakini ninaamini hatua tuliyofikia ni muhimu na inayokwenda kubadili klabu yetu,”amesema Manara.
Mfanyabiashara mashuhuri na mwanachama wa klabu hiyo Mohammed Dewji alitangaza kununua asilimia 50 za hisa za klabu hiyo akilenga kuipaisha ili iweze kushindana na klabu nyingine kubwa barani Afrika zikiwemo TP Mazembe, Al Ahly na Mamelod Sundowns.
Simba ilianzishwa mwaka 1936 na ni klabu inayoongoza kwa kuwa na mafanikio katika ukanda wa Afrika Mashariki kwakuwa imetwaa mara sita taji la Kagame Cup.