Connect with us

 

Simba wameongeza matumaini ya kunyakua taji la soka katika ligi ya Tanzania bara baada ya kuwashinda watani wao wa jadi Yanga kwa mabao 2-1 Jumamosi jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Yanga ilipata bao lake la ufunguzi katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Simon Msuva kupitia mkwaju wa penalti, katika dakika ya tano ya mchuano huo.

Kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza, Yanga walikuwa wanaongoza lakini kipindi cha pili, mambo yalibadilika baada ya Laudit Mavugo kusawazisha.

Simba wakiwa wachezaji 10 baada ya Janvier Bokungu kupewa kadi nyekundu, walijihakikishia ushindi kupitia mkwaju wa Shiza Kichuya kuelekea mwishoni mwa mchuano huu.

Matokeo haya yanaendelea kuiwekea Simba katika nafasi ya kwanza kwa alama 54 huku Yanga ikiwa ya pili kwa alama 49.

Uchambuzi zaidi

Simba

Simba inaongoza ligi kwa alama 51 baada ya mechi 23, imeshinda mechi 17, imetoka sare mara tatu na kupoteza mechi tatu.

Kocha wa klabu hii ni Joseph Omog raia wa Cameroon, kabla ya kuanza kuifunza Simba, mwaka 2013 aliwahi kuifunza Azam FC lakini pia ni kocha wa zamani wa AC Leopard ya Congo Brazaville.

Yanga

Mabingwa watetezi wa ligi kuu. Wanaendelea kuwa katika nafasi ya pili kwa alama 49, baada ya mechi 22.

Wana mechi moja kiporo kutokana na mchezo wa Kimataifa wa klabu bingwa barani Afrika.

Kocha wa klabu hii ni George Lwandamina, kutoka Zambia kuanzia mwaka uliopita. Aliwahi pia kuwa kocha wa ZESCO United, Red Arrows, Kabwe Warrios, Mufulira Wanderers zote za Zambia lakini pia amewahi kuwa kocha wa timu taifa ya Zambia.

Wamefunga mabao 47, na inakuwa klabu iliyofunga mabao mengi katika michuano yao yote hadi leo hii.

Imeshinda mechi 15, imetoka sare mara nne na kupoteza michezo mitatu.

Rekodi ya vlabu hivi viwili toka mwaka 2013.

20/10/13 Simba 3-3 Yanga

19/04/14 Yanga 1-1 Simba

18/10/14 Yanga 0-0 Simba

08/03/15 Simba 1-0 Yanga

26/09/15 Simba 0-2 Yanga

20/02/16 Yanga 2-0 Simba

01/10/16 Yanga 1-1 Simba

25/02/2017 Simba 2-1 Yanga

 

More in East Africa