Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imemfukuza kazi Kocha Joseph Omog, siku moja baada ya kuvuliwa ubingwa wa michuano ya Kombe la FA kwa kufungwa na timu ya daraja la pili ya Green Worriers.
Taarifa ya klabu ya Simba iliyotolewa jioni hii inasema uongozi wa klabu hiyo na Omog kwa pamoja wameamua kuvunja mkataba na kwamba kwa sasa timu itaendelea kuwa chini ya Kocha Msaidizi Mrundi, Masoud Djuma.
Omog alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea nyumbani kwao nchini Cameroon.Aliwahi kuifundisha Azam na kuipa ubingwa wa Tanzania Bra msimu wa 2013/14.
Tetesi za kufukuzwa kazi Omog zilianza kuzagaa jana baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya FA.
Simba ni klabu pekee nchini Tanzania iliyotumia gharama kubwa kufanya usajili msimu huu ikiwemo kumsajili nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima aliyekuwa anaichezea Yanga na mshambuliaji wa Uganda Emmanuel Okwi aliyekuwa anaitumikia SC Villa.
Mwkezaji mpya wa Simba, Tajori Mohammed Dewji mapema leo aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kumtaka Omog aachie ngazi kutokana na Madrid.
Kocha huyo amefukuzwa kazi huku mkataba wake ukiwa umebaki miezi sita kumalizika.