Na Fredrick Nwaka,
Dar es Salaam. Wajumbe wa mkutano mkuu wa kawaida wa klabu ya Simba wamepitisha pendekezo la kumsimamisha uanchama Mzee Hamis Kilomoni.
Azimio hilo limefikiwa katika mkutano wa wanachama uliofanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere Mjini Dar es Salaam.
Kilomoni, mchezaji na kiongozi wa zamani wa klabu hiyo alikuwa mstari wa mbele kupinga kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo na alifikia hatua ya kufungua kesi mahakamani akipingia uwepo wa mkutano wa leo.
Viongozi wa Simba wamesema watamwandikia barua ya Mzee Kilomoni ili atoe utetezi wake.
“Tumemsaimamish na atapewa barua ili ajitete kwanini ameipeleka klabu mahakamani,”alisema Haji Manara, Ofisa Mawasiliano wa Simba.
Katika mchakato wa kubadili mfumo wa uendeshaji, Mfanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania Mohammed Dewji amepanga kununua hisa asilimia 51 kwa bilioni 20 za Tanzania.
Mkutano wa leo pia umemchagua Waziri wa zamani Profesa Juma Kapuya na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoi kuwa wadhamini wa klabu hiyo.