-
-
by
Victor Abuso
Vlabu mbalimbali vya soka Tanzania bara, viliandikisha matokeo mbalimbali wakati wa michuano ya mwishoni mwa juma lililopita huku mabingwa wa zamani, Simba, Azam na mabingwa watetezi wakipa ushindi.
Simba3 Kagera Sugar 1
Mabingwa wa zamani Simba FC kutoka mitaa ya Msimbazi jijini Dar es salaam wakiwa katika uwanja wa taifa ,walipata ushindi mkubwa wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Kagera Sugar kutoka Bukoba.
Mchezaji wa Kimataifa kutoka Uganda Hamis Kiiza aliipa timu yake mabao yote matatu na kuwa nyota wa mchezo huo, huku Mubarak Yusuf akiipa Kagera bao pekee la kufuta machozi.
Ushindi huu unaonesha maandalizi ya klabu ya Simba inayotafuta ubingwa msimu huu na mwishoni mwa juma hili watacheza na watani wao wa jadi Yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Wakati timu hizi mbili zinapokutana, mashabiki huvutana sana kuhusu mshindi wa mchuano huo.
Azam 1 Mwadui 0
Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC nao walipata wakati mgumu mbele ya Mwadui FC kwa kupata bao 1 kwa 0.
Bao la pekee la Azam lilitiwa kimyani na John Bocco.
Matokeo mengine ya mwishoni ni kati ya Mtimbwa Sugar waliopata ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Ndanda FC, huku Coastal Union wakitoka sare ya kutofungana na Toto Africans.
Siku ya Jumamosi, Yanga FC waliwapa ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa 1 dhidi ya JKT Ruvu jijini Dar es salaam.
Kwa matokeo hayo, Yanga na Simba ambao wameshinda mechi zao zote tatu za ufunguzi wanachuana katika msururu wa ligi nchini humo kwa alama 9 kabla ya mchuano wa Jumamosi.
Azam FC mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati pia wana alama tatu wamepata ushindi katika michuano yao ya ufunguzi sawa na Mtibwa Sugar inayoshikilia nafasi ya nne.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...