Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Uongozi wa Simba SC leo umemtangaza aliywahi wahi kuwa kocha msaidizi wa Cameron Sven Vanderbroeck ,40, raia wa Ubelgiji kama kocha mkuu.
Simba SC ambayo imemfuta kazi kocha wake Patrick Aussems Novemba 30 2019 umemuajiri Sven lakini imefanya siri makubaliano ya muda waliyompa katika mkataba.
Inadaiwa kuwa Simba wamempa Sven mkataba usiozidi mwaka kwani wanataka wajiridhishe na uwezo wake kwanza kwani amekuwa hana rekodi nzuri sana toka awe kocha mkuu.
Sven aliwahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Cameroon iliyoshinda Ubingwa wa AFCON 2017 nchini Gabon na alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia kwa kipindi cha mwaka mmoja (2018-2019).