Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kesho itamenyana na Benin katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa katika Jiji la Cotonou nchini humo.
Mchezo huo ni wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya Fifa na tayari Tanzania ilishawssili nchini Benin kwa ajili ya mchezo huo muhimu kwa ajili ya kuska viwango vya Shirikisho la Soka Duniani.
Stars itamkosa nahodha wake Mbwana Samatta anayeichezea KRC Genk ya Ubelgiji ambaye aliumia mguu wiki iliyopita, jeraha litakalomweka nje hadi mwezi januari.Hata hivyo Kocha Salum Mayanga amesema atatumia wachezaji wengine kuziba nafasi yake.
Katika mchezo huo Stars itategemea baadhi ya wachezaji wake muhimu wanaocheza nje akiwemo Abdi Banda anayecheza Baroka FC ya Afrika Kusini, Farid Mussa wa Tenerife ya Hispania na kiungo Hamis Abdallah anyecheza soka nchini Kenya kwenye kikosi cha Sony Sugar.
Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa, Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.