Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars, imepiga kambi nchini Afrika Kusini kwa muda wa siku 10 kujiandaa kwa mchuano muhimu wa kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Tanzania itamenyana na Algeria na tarehe 14 mwezi huu katika mchezo wa mzunguko wa pili, huku mchuano wa kwanza ukichezwa nyumbani jijini Dar es salaam na ule wa pili kuchezwa siku tatu baadaye jijini Algiers.
Kocha wa Taifa Stars Charles Mkwasa licha ya kushangazwa lakini amefurahishwa na mabadiliko ya dakika za mwisho kwa timu yake kwenda Afrika Kusini, badala ya Oman kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Mkwasa ameandamana na wachezaji 24 wanaocheza soka nyumbani walioitwa kambini wiki iliyopita.
Washambuliaji wa Kimataifa wanaocheza soka katika klabu ya TP Mazembe Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta pamoja Mrisho Ngassa anayecheza soka katika klabu ya Free Stars watajiunga na kikosi hicho siku tatu au nne kabla ya kuondoka nchini Afrika Kusini.
Kikosi kamili:
Makipa: Ali Mustafa, Aishi Manula and Saidi Mohamed, all goalkeepers.
Mabeki: Juma Abdul, Haji Mwinyi, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Hassan Kessy, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Salim Mbonde, Hassan Isihaka.
Viungo wa Kati: Salum Telela, Himid Mao, Jonas Mkude, Salum Abubakari, Saidi Ndemla, and Frank Domayo.
Washambuliaji: Simon Msuva, Farid Mussa, Malimi Busungu, John Bocco and Ibrahim Ajibu.