Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema timu yake inaingia katika mchezo wa kesho dhidi ya Rayon Sports ikiwa na wachezaji wake mahiri Obrey Churwa na Amis Tambwe.
Wachezaji hao wamekuwa nje kwa muda kutokana na majeraha.
Yanga na Rayon Sports zitachuana siku ya Jumatano katika nchezo wa hatua ya makundi ya taji la shirikisho ikiwa ni ya pili kwa kila timu.
“Chirwa na Tambwe wako fiti lakini pia Kamusoko, kuhusu Ajibu, nadhani bado hayuko sawasawa”amesema Mwandila.
Kocha huyo amesema hawatawadharau wapinzani wao kutokana na wao pia kuwa washindani katika muchuano hii.
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub amesema timu yake haina cha kupoteza katika nchezo huo baada ya kufanya vibaya katika Ligi Kuu.
“Kila mchezaji analijua hilo. Mechi ya kesho ni ngumu na tunawaheshimu wapinzani wetu. Ushindi wa kesho utatupatia nguvu kama wachezaji na pia mashabiki wetu. Tunacheza nyumbani lazima tushinde.
Kocha wa Rayon Sports Ivan Minnaert amesema timu yake inaiheshimu Yanga na itaingia uwanjani kutafuta matokeo.
Yanga ilianza vibaya hatua ya makundi kwa kufungwa mabao 4-0 na USM Alger wakati wapinzani wao Rayon Sports walianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi y Gor Mahia ya Kenya.
Ripoti ya Fredrick Nwaka