Connect with us

Tanzania kuwa wenyeji wa michuano ya vijana wasiozidi miaka 17

Tanzania kuwa wenyeji wa michuano ya vijana wasiozidi miaka 17

Na Victor Abuso,

Shirikisho la soka barani Afrika CAF limeiteua Tanzania kuwa mwenyeji wa michuano ya vijana chipukizi wasiozidi miaka 17 mwaka 2019.

Mwenyekiti wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Jamal Malinzi amesema uongozi wa soka umefurahishwa na uamuzi wa CAF.

Kuwa wenyeji wa michuano hii ya vijana barani Afrika ni ishara kuwa ipo siku tutaanda michuano ya mataifa bingwa barani Afrika AFCON siku zijazo,” alisema.

Jamal ameongeza kuwa hii ni changamoto kwa Shirikisho hilo kuanza kuandaa kikosi kitakachoshiriki katika michuano hiyo lakini kwanza ni kuunda kikosi cha wachezaji wasiozidi miaka 13 watakaoshiriki katika michuano ya Afrika mwaka 2015.

Habari hii kutoka CAF imepokelewa kwa furaha kubwa na wadau wa soka nchini humo ambao wanasema Tanzania sasa ina nafasi ya kuonesha vipaji vyake na uwezo wa kuwa wenyeji wa michuani hii mikubwa barani Afrika.

Tanzania inajivunia uwanja wa kisasa wa Taifa jijini Dar es salaam, ule Chamazi nje kidogo jiji la Dar es salaam na CCM Kirumba mjini Mwanza.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in