Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Sare ya 0-0 ya mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Rwanda, Kigali Rwanda inatoa picha tofauti kuelekea mchezo wa Tanzania dhidi ya Sudan wa kuwania kucheza fainali za CHAN 2020 zitakazofanyika nchini Cameroon.
Mchezo wa Tanzania dhidi ya Rwanda ulikuwa ni wa kimataifa wa kirafiki unaotambulika na FIFA, ila ilikuwa ni kipimo pia wachezaji wa Tanzania wanaotarajia kucheza mchezo wa CHAN 2020 hususani safu ya ushambuliaji inayoonekana kuwa butu.
Kufuatia kupoteza 1-0 mchezo wa Septemba 22 wa kwanza dhidi ya Sudan uwanja wa Taifa, Tanzania inahitaji ushindi wa kuanzia magoli mawili kwenda juu Oktoba 19 jijini Khartoum ila safu ya ushambuliaji hairidhishi hadi sasa haina goli hata moja ndani ya dakika zote 270 ya michezo yote mitatu ya CHAN 2020.
Taifa Stars chini ya Ndairagije imecheza jumla ya michezo sita (mitatu kati ya hiyo ya CHAN 2020) pamoja na leo dhidi ya Rwanda ikiwa imefunga jumla ya 6mabao 2 na kufungwa matatu, hayo magoli mawili moja lilifungwa na Simon Msuva anayecheza soka Morocco katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar na lingine lilifungwa na Samatta katika sare ya 1-1 dhidi ya Burundi mchezo wa marudiano jijini Dar es salaam wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Tunaita ni mtihani utakuwepo jijini Khartoum ni kutokana na Tanzania hadi sasa kikosi chake cha kuwania kufuzu CHAN 2020 hakijafunga bao lolote ndani ya dakika 90 ikicheza michezo mitatu, hivyo kufunga kwa Msuva na Samatta kunaonesha kabisa kwa kikosi cha CHAN Tanzania haina wafungaji.
Samatta na Msuva wanacheza Ligi za nje hivyo CHAN hawatokuwepo ndio maana Tanzania itakuwa na mtihani mzito zaidi ikienda ugenini kutafuta ushindi na kulinda goli ila kwa safu ya ushambuliaji kikosi cha CHAN ni wazi butu licha ya wanaotajiwa kucheza dhidi ya Sudan wamejaribiwa katika mchezo dhidi ya Rwanda lakini bila mafanikio.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...