Tanzania ilianza vema michuano ya soka kuwania ubingwa wa COSAFA baina ya mataufa ya Kusini mwa bara Afrika iliyoanza jana nchini Afrika Kusini kwa kuishinda Malawi mabao 2 kwa 0.
Huu ndio ushindi wa kwanza kwa Tanzania ambao wamealikwa katika mashindano haya, baada ya kujaribu kufanya hivyo mwaka 1997 na 2015.
Mabao yote ya Tanzania yalitiwa kimyani na mchezaji Yahya Ramadhani.
Angola nao walianza vema kwa kuishinda Mauritius bao 1-0 lililofungwa na Augusto Quibeto katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.
Tanzania inaongoza kundi la A kwa alama 3 mbele ya Angola ambayo pia ina alama tatu lakini tofauti ya bao moja.
Mshindi wa kundi hili atamenyana na Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali.
Ratiba ya kundi B:
- Msumbiji vs Zimbabwe
- Madagascar vs Ushelisheli
Mshindi wa kundi hili atapambana na Swaziland katika hatua ya robo fainali tarehe mbili mwezi Julai.