-
-
by
Victor Abuso

Tanzania imeandikisha historia baada ya kufuzu katika fainali ya bara Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 38, kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya kufuzu ya kundi L, iliyochezwa Jumapili jioni jijini Dar es salaam.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na wachezaji Simon Msuva katika dakika ya 21 ya mechi hiyo, huku beki Erasto Nyoni akifunga bao la pili kupitia mkwaju wa penalti.
Agrey Moris naye alihakikisha Tanzania inapata ushindi wa kuridhisha, baada ya kuifunga Taifa Stars bao la tatu katika dakika 57, kupitia shambulizi la kichwa lililomwacha kipa wa Uganda Dennis Onyango akishindwa kuokoa shambulizi hili.
Mara ya mwisho kwa Tanzania kufuzu katika fainali za AFCON ilikuwa ni mwaka 1980 nchini Nigeria na imefuzu nchini Misri, chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.
Wachezaji wote wa Taifa Stars waliocheza mechi za hatua ya makundi kufuzu kuelekea Misri, walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho nchi yao iliposhiriki katika michuano ya bara Afrika.
Licha ya kufungwa, Uganda imefuzu katika fainali hiyo ikiwa inaongoza kundi hilo kwa alama 13, huku Tanzania ikiwa ya pili kwa alama nane.
Kutofungana kwa Cape Verde na Lesotho, jijini Praia pia kumeisaidia Tanzania kufuzu.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...