Kamati inayosimamia uchaguzi wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF imetangaza tarehe mpya za kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa soka nchini humo.
Uchaguzi wa matawi utafanyika tarehe 14 na tarehe 26 mwezi huu wa Januari huku ule wa kitaifa ukipangwa kufanyika tarehe 10 mwezi wa Februari.
Uchaguzi huu ulisitishwa mwishoni mwa mwaka uliopita, baada ya kuwepo kwa madai ya udanganyifu na wizi wa kura na hivyo kusitisha zoezi hilo katika maeneo yaliyoathiriwa.
Kamati hiyo inaahidi kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki na washindi halali ndio watakaotangazwa .
Hii ni mara ya tatu kwa uchaguzi huu kuahirishwa wakati huu wagombea wa wadhifa wa urais wa FKF wakiendelea na kampeni kuomba kura kwa wajumbe wa soka nchini humo.
Rais wa sasa wa FKF Sam Nyamweya anatetea wadhifa wake lakini anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia Ambrose Rachier na Mwenyekiti wa klabu ya Kariobangi Sharks Nick Mwenda.