Shirikisho la Soka Tanzania TFF limeandika barua wizara ya habari utamaduni sanaa na michezo ili kuomba rais Magufuli kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imepangwa kufanyika Jumamosi katika Uwanja wa Taifa.
Kauli ya TFF kuandika barua hiyo imetolewa na Rais wa TFF Wallace Karia alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari leo, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Karia tukio la Rais Magufuli kukabudhiwa kombe endapo atakubali mwaliko huo litafanyika Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, siku ambayo Simba itacheza na Kagera Sugar katika nchezo wa Ligi Kuu.
“Waziri Mwakyembe pia amesema analifanyia kazi barua yetu na tunaamini ni sahihi kumkabidhi Myeshimiwa Rais Kimbehili,*amesema Karia.
Serengeti Boys ilitwaa ubingwa katika michuano ya Vijana chini ya miaka 17 iliyofanyika nchini Burundi kwa kuifunga Somalia mabao 2-0.
Aidha, Karia amesema katika ombi hilo pia TFF imemualika Rais Magufuli kukabidhi kombe la Ligi Kuj kwa mabingwa wapya Simba.
“Ni matumaini yetu mchezo huo utaanza saa nane mchana, na huu ni mwaka wetu wa kwanza kusimamia ligi tumepanga kila kitu kiende sawa, “amesema Karia.
Simba ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kufikisha alama 68 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.