Connect with us

TFF yaongeza muda wa kuwasajili wachezaji

TFF yaongeza muda wa kuwasajili wachezaji

Na Victor Abuso

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, limeongeza muda wa kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji wanaocheza katika ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Siku ya mwisho ya kuwasajili wachezaji hao itakuwa ni tarehe 20 mwezi huu wa Agosti katika ligi kuu, ligi ya Daraja la kwanza na ligi ya daraja la pili.

Muda wa mwisho ulikuwa unatarajiwa kufungwa tarehe 6 mwezi huu huku ule usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba tarehe 5 na sasa usajili wa ujumla utamalizika tarehe 20.

Uongozi wa soka nchini humo umeongeza kuwa kati ya tarehe 21 na 28 utakuwa ni kipindi cha pingamizi.

TFF imevitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda huo uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za lala salama.

Ligi kuu ya Tanzania bara itarajiwa kuanza katikati ya mwezi Septemba huku usajili wa dirisha dogo ukitarajiwa kufanyika tarehe Novemba 15.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in