Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Thomas Ulimwengu amejiunga na klabu ya Al Hilal ya Sudan baada ya kuachwa na klabu ya Elskistuna ya Sweden. Amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Kwa muda mrefu mchezaji huyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na maumivu yaa goti na alishindwa kudumisha kiwango chake tangu alipoihama TP Mazembe mwaka 2016.
Timu hiyo imeshika nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi nchini humo ikiwa imejikusanyia pointi 33 katika michezo 33 iliyocheza.
Ulimwengu amejiunga na Al Hilal baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza soka tangu aachane na timu ya AFC Eskilstuna ya Sweden aliyokuwa akiitumikia.
Winga huyo pia aliwahi kuitumikia klabu ya TP Mazembe ya Congo sambamba na Mshambuliaji Mtanzania mwenzake anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji hivi sasa, Mbwana Samatta.