Mechi za timu za taifa za mchezo wa soka kufuzu kwa fainali ya mwaka 2019 kwa wachezaji wasiozidi miaka 23 barani Afrika, zinachezwa kuanzia siku ya Jumatano.
Mataifa nane yatafuzu kushiriki katika fainali hiyo, itakayochezwa nchini Misri mwezi Novemba mwaka 2019. Nigeria ndio mabingwa watetezi.
Mashindano ya bara Afrika kufanyika kila baada ya miaka minne.
Timu tatu bora, zitafuzu katika fainali ya michezo ya Olimpiki nchini Japan mwaka 2020.
Afrika Kusini,Zimbabwe, Zambia, Congo Brazzaville, Gabon, Algeria, Sierra Leone, Tunisia, Ivory Coast, Senegal, Nigeria, Morocco na Mali zimefuzu katika hatua ya pili ya michuano hii.
Ratiba ya mzunguko wa kwanza, mechi za kufuzu katika fainali hiyo ya Afrika ni pamoja na:-
Jumatano:
Jijini Bujumbura, Bujumbura
Burundi v Tanzania
Jijini Addis Ababa
Ethiopia v Somalia
Jijini Nairobi
Kenya v Mauritius
Mjini Rubavu, Rwanda
Rwanda v DRC
Jijini Victoria
Ushelisheli v Sudan
Jijini Kampala
Uganda v Sudan Kusini
Jijini Nouakchott
Mauritania v Guinea
Jijini Malabo
Equatorial Guinea v Sao Tome e Principe
Ijumaa
Jijinii Yaounde
Cameroon v Chad
Jijini Luanda
Angola v Namibia
Mjini Kumasi, Ghana
Ghana v Togo
Jijini Maputo
Mozambique v eSwatini
Jijini Ouagadougou
Burkina Faso v Niger