-
-
by
Victor Abuso
Mabingwa wa zamani wa taji la klabu bingwa barani Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inachuana na Stade Gabesien ya Tunisia katika mchuano wa mzunguko wa kwanza kutafuta nafasi ya kufuzu katika hatu ya makundi, kusaka taji la Shirikisho barani Afrika.
Mazembe ambao walishinda taji la klabu bingwa msimu uliopita, wanashiriki katika mashindano haya baada ya kuondolewa katika hatua ya mwondoano na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco katika harakati ya kutetea taji lake.
Mchuano huu unachezwa katika uwanja wa Kamalondo mjini Lumbubashi kuanzia saa 11 na nusu jioni saa za Afrika Mashariki.
Mashabiki wa Mazembe wanatumai kuwa wachezaji wa klabu yao watawapa furaha baada ya huzuni ya mwezi uliopita katika michuano ya klabu bingwa.
Michuano mingine kama hii ilichezwa jana Jumamosi.
Matokeo mengine ya siku ya Jumamosi:-
- Yanga (Tanzania) 2 Sagrada Esperanca (Angola) 0
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) 3 Medeama (Ghana)1
- Mo Bejaia (Algeria) 0 Esperence de Tunis(Tunisia) 0
- Stade Malien Bamako (Mali) 0 FUS Rabat (Morocco ) 0
- Al Merreikh (Sudan) 1 Kawkab Marrakech (Morocco) 0
Michuano ya mzunguko wa pili itachezwa baada ya wiki mbili na washindi kufuzu katika hatua ya makundi.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...