-
by
Victor Abuso
Michuano ya marudiano hatua ya mwondoano katika mchezo wa soka kuwania ubingwa wa taji la Shirikisho inachezwa leo na kesho katika mataifa mbalimbali barani Afrika.
Mabingwa wa mwaka uliopita wa klabu bingwa barani Afrika TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inamenyana na Stade Gabesien ya Tunisia.
Mazembe inayofuzwa na Mfaransa Hubert Velud, inakwenda katika mchuano huu ikiwa na ushindi wa bao 1 kwa 0 waliopata katika mchezo wa nyumbani mapema mwezi huu.
Mashabiki wa TP Mazembe wana imani kuwa klabu yao itawafuta machozi kwa kupata ushindi leo na kufuzu katika hatua ya makundi na kufika hadi fainali kunyakua ubingwa wa taji la Shirikisho baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa.
Klabu hii yenye makao yake mjini Lubumbashi inajivunia wachezaji kutoka nchi mbalimbali kutoka barani Afrika kama Ghana, Ivory Coast, Mali, Tanzania na Zambia. Mechi hii itapigwa kuanzia saa kumi na nusu jioni saa za Afrika Mashariki.
Mchuano mwingine unaochezwa leo ni kati ya Mo Bejaia ya Algeria mabyo itakuwa ugenini kumenyana na Esperance de Tunis ya Tunisia.
Mchuano wa kwanza, timu zote mbili zilitoka sare ya kutofungana. Mchuano huu utachezwa kuanzia saa mbili na nusu usiku saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya kesho na matokeo ya mzunguko wa kwanza:-
- Stade Malien (Mali) vs FUS Rabat (Morroco) 0-0
- Etoile du Sahel (Tunisia) vs CF Mounana (Gabon) 2-0
- Al-Ahli Tripoli (Libya) vs Misr Lel Makkasa (Misri) 0-0
- Al-Merrikh (Sudan) vs Kawkab Marrakech( Morroco) 1-0
- Young Africans (Tanzania) vs Sagrada Esperanca (Angola) 2-0
- Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) vs Medeama (Ghana) 3-1
Timu nane zitafuzu katika hatua ya makundi.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...