Connect with us

TP Mazembe kutafuta heshima dhidi ya Wydad Casablanca

TP Mazembe kutafuta heshima dhidi ya Wydad Casablanca

 

Mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Afrika CAF, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco kutafuta tiketi ya kufuzu katika hatua ya makundi mjini Lubumbashi.

Mazembe wana kazi kubwa kwa sababu katika mchuano wa mzunguko wa kwanza wiki mbili zilizopita, walipoteza mchuano huo kwa kufungwa mabao 2 kwa 0.

Kocha Hubert Velud amenukuliwa akisema anatambua kazi kubwa iliyo mbele yake lakini vijana wake watafanya kile wanachoweza kupata ushindi nyumbani.

Mazembe wanastahili kupata angalau mabao mabao 3 kwa 0 ili kusonga mbele na ikiwa itaondolewa katika michuano hii, itakwenda kucheza katika hatua ya mwondoano katika taji la Shirikisho.

Mchuano mwigine unaofuatiliwa Afrika Mashariki na Kati ni ule wa ya Yanga FC ya Tanzania na Al-Ahly ya Misri.

Mchuano wa kwanza uliochezwa jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita, timu zote mbili zilitoka sare ya bao 1 kwa 1.

Hii inamaana kuwa ikiwa Yanga inataka kusonga mbele, ni lazima ipate ushindi huko Misri lakini historia ya soka imeendelea kuwa mbaya kati ya vlabu vya Afrika Mashariki na vile vya Afrika Kaskazini imekuwa ikiipendelea vlabu vya nchi za kiarabu.

Mbali na hayo, Zamalek ya Misri, Zesco United ya Zambia na ES Setif ya Algeria zimekuwa klabu za kwanza kufuzu katika hatua ya makundi baada ya ushindi siku ya Jumanne usiku.

Matokeo:

  • ES Setif 2 Al-Merrikh 2 -Es Setif ilifuzu kwa sababu ya bao la ugenini
  • Zamalek 3 MO Bejaia 1
  • Zesco 5 Stade Malien 2

Ratiba Kamili:-

  • AS VITA Club vs Mamelodi Sundowns
  • Wyadad Casablanca vs TP Mazembe
  • Enyimba vs Etoile du Sahel
  • Young Africans vs Al-Ahly
  • ASEC Mimosas vs Al-Ahli Tripoli

Michuano ya taji la Shirikisho pia inachezwa siku ya Jumatano:-

  • MC Oran vs Kawakab Marrakech
  • CS Constantine vs Misr El-Makasa
  • Al-Ahly Shendi vs Medeama
  • FUS Rabat vs SC Villa
  • CF Mouna vs ENPPI

Klabu ya Azam FC ya Tanzania imeondolewa katika michuano hii baada ya kufungwa na Esperance de Tunis ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4 kwa 2.

Wiki mbili zilizopita, Azam ikicheza jijini Dar es salaam ilipata ushindi wa mabao 2 kwa 1 lakini ikashindwa kuulinda ugenini.

Matokeo mengine:-

  • Vita Club Mokanda 1 Sagrada Esperenca 4
  • Zanaco 1 Stade Gabesien 4

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in