Connect with us

 

Tusker FC ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya soka nchini Kenya.

Ubingwa wa Tusker FC, klabu yenye makao yake katika mtaa wa Ruaraka jijini Nairobi, umekuja baada ya kuifunga AFC Leopards bao 1-0 na kunyakua alama tatu muhimu katika mchuano uliochezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

Tusker FC ilihitaji ushindi kutawazwa mabingwa kwa sababu wanaongoza ligi kwa alama 58 na hata wakishindwa mechi ya mwisho wataendelea kuwa mabingwa.

Gor Mahia inamaliza nafasi ya pili, licha ya kuwa katika harakati za kutetea taji waliloshinda mara tatu mfululizo kutofua dafu, na ni pili kwa alama 54.

Michuano wa mwisho utawakutanisha mabingwa hawa wapya na mabingwa wa zamani Gor Mahia jijini Nairobi wiki ijayo, wakati ligi itakapokamilika rasmi.

Tusker FC sasa imeshinda taji hili mara 11, mwaka 1972,1977,1978,1994,1996,1999,2000,2007,2011,2012 na 2016.

Gor Mahia bado inashikilia rekodi ya ubingwa nchini humo kwa kunyakua mataji 15 ikiwa ni pamoja na kushinda taji hilo mara tatu mfululizo mwaka 2013, 2014 an 2015.

Tusker FC sasa itawakilisha Kenya katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika mwaka ujao pamoja na taji la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA.

More in