Timu ya taifa ya soka ya Ubelgiji imekuwa ya kwanza barani Ulaya kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Hatua hii imekuja baada ya Ubelgiji kuishinda Ugiriki katika mechi muhimu dhidi ya Ugiriki kwa mabao 2-1.
Bao la mshambuliaji Romelu Lukaku katika dakika ya 74 ya mchuano huo, lilitosha kuisaidia nchi yake kufuzu katika fainali hiyo muhimu kutoka kundi H.
Kati ya mechi nane ilizocheza, Ublegiji imeshinda mechi saba kutoka sare mara moja lakini haijapoteza mchuano wowote na hivyo inaongoza kundi hili kwa alama 22 mbele ya Bosnia-Herzegovina ambayo ina alama 14.
Mbali na Ubelgiji, timu ya taifa ya Ufaransa ilishindwa kupata alama tatu muhimu baada ya kutofungana na Luxembourg nyumbani.
Matokeo haya yamewashangaza wapenzi wa soka nchini Ufaransa na ndio mara ya kwanza kwa Ufaransa kushindwa kuifunga Luxembourg tangu mwaka 1914.
Matokeo mengine:-
Hungary 0-1 Ureno
Latvia 0-3 Switzerland
Uholanzi 3-1 Bulgaria
Belarus 0-4 Sweden