Uchaguzi wa Shirikisho la soka nchini Sudan Kusini uliokuwa umepangwa kufanyika mwisho wa mwezi huu, umeahirishwa kwa sababu za kisiasa.
Rais wa zamani Chabur Goc Alei, amedai kuwa Kamati itakayosimamia Uchaguzi huo, imeonekana ikipata ushawishi kutoka kwa wabunge na Magavana wa chama tawala chama, kwa madai kuwa wanataka mgombea wao.
Mbali na Chabur, kuna ripoti ya baadhi ya wanachama wa Kamati kuu wameliandikia barua Shirikisho la soka duniani FIFA, kulalamikia suala hili.
Wadau wa soka nchini Sudan Kusini sasa wanaiomba FIFA kusaidia kuandaa Uchaguzi huu .
Uchaguzi huu unatarajiwa kufanyika baada ya Chabur, kuondolewa katika wadhifa huo kwa madai ya ufisadi na baadaye akaamua kujiuzulu.
Adelmo Wani Agustino kwa sasa ndiye rais wa SSFA.
Shirikisho la soka nchini humo SSFA, kilizinduliwa mwaka 2012 na baadaye kujiunga na FIFA, CAF na CECAFA.