Connect with us

 

Mkutano wa marais saba wa vyama vya soka kutoka ukanda wa CECAFA waliokutana jijini Kampala nchini Uganda na kukubaliana mambo tisa ya kuimarisha soka na kuleta mabadiliko ya uongozi, umezua maswali mbalimbali kutoka kwa wadau wa soka ikiwa walifuata utaratibu wa kukutana.

Swali kuu linaloendelea kuzua mjadala inakuwaje kuwa mkutano huo uliendelea bila ya kuwepo kwa mwakilishi hata mmoja kutoka ukanda wa CECAFA, kwa sababu maswala yaliyikuwa yanazungumzwa yalikuwa ni ya ukanda.

Taarifa iliyotolewa na viongozi hao baada ya kukuatana ni kuwa, walimwalika Katibu MkuuNicholas Musonye ambaye hakujibu mwaliko wao lakini pia rais wa Baraza hilo Mutasim Jaffar ambaye alisema hakuwa na muda wa kuja Kampala.

Marais waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na mweyeji wao Moses Magogo, Vincent Nzamwita kutoka Rwanda, Jamal Malinzi (Tanzania), Juneidi Tilmo (Ethiopia), Nicolas Mwendwa (Kenya), Ndikuniyo Reverien (Burundi) na Ravia Faina kutoka Zanzibara.

Mambo mawili muhimu kati ya tisa yaliyokubaliwa kati yao ni pamoja na kuitisha mkutano mkuu wa CECAFA haraka iwezekanavyo na kuibadilisha Katiba ya Baraza hilo.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Ugands FUFA Moses Magogo, amesema lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kujadiliana namna ya kuimarisha soka na kutafuta fedha, wala sio kushiriki katika siasa za soka.

Kanuni ya CECAFA hatan hivyo inaeleza wazi kuwa Katibu Mkuu ambaye kwa sasa ni Musonye ndiye Mtendaji Mkuu.

Anawajibika kusimamia shughuli zote za Baraza hilo ikiwa ni pamoja na kuitisha mikutano baada ya kupata idhini kutoka kwa rais.

Aidha, amepewa mamlaka ya kuandaa ajenda za mkutano wowote unaozungumzia soka la ukanda na mambo mengine muhimu.

Wachambuzi wa soka wanasema kwa kuangalia kanuni, marais hao hawakufuata utaratibu lakini hatua hii huenda imesukumwa na kimya cha muda mrefu cha viongozi wa CECAFA.

Mwaka 2016 michuano ya kila mwaka, klabu bingwa na baina ya mataifa hayakufanyika kwa sababu ya ukosefu wa mweyeji na mfadhili.

Uongozi wa CECAFA miaka ya hivi karibuni imeendelea kukabiliana na changamoto kubwa za kupata wafadhili ili kufanikisha michuano hii.

More in CECAFA Women's Senior Challenge