Hatua ya Lionel Messi kunyakua taji la mchezaji bora katika mchezo wa soka duniani kwa mara ya tano na kuweka historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kuwahi kufikia kiwango hicho, inaweka wazi mafanikio ya mshambuliaji huyu matata.
Messi mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina, alianza kuichezea Barcelona mwaka 2001 akiwa kijana chipukizi na hadi sasa bado anakipiga na klabu hiyo.
Kuendelea kuichezea Barcelona kumemjenga na kumfanya kuwa na nidhamu nje ya ndani ya uwanja.
Unyenyekevu wa Messi pia umemsaidia katika uchezaji wake na hata alipotangazwa mshindi alionekana mtulivu na hata kuwapa mkono wenzake, Neyma na Christiano Ronaldo.
Baada ya kutangazwa mshindi, Messi alikuwa na haya ya kusema:-
“Tumeendelea kuwa na uhusiano mzuri na Ronaldo,”.
“Wote tunacheza soka, tuna changamoto za kila siku licha ya kuchezea timu tofauti, na hizi tofauti tunazozisikia zinaangaziwa na wanahabari ,”.
Messi amekuwa mfungaji bora katika ligi kuu nchini Uhispania La Liga mara 3, msimu wa mwaka 2009-2010 alifunga mabao 34, 2011-2012 akafunga mabao 50 na msimu wa mwaka 2012-2013 alifunga mabao 46.
Amewahi pia kuongoza katika ufungaji wa mabao katika michuano ya klabu bingwa mara tano, mwaka 2008-2009 alifunga mabao 9, 2009-210 mabao 8, 2010-2011 mabao 12, mwaka 2011-2012 mabao 14 na mwaka 2014-2015 mabao 10.
Messi ameisaidia klabu yake kushinda mataji yafuatayo:
- Klabu bingwa barani Ulaya mara 4 : 2005-06, 2008-09, 2010-11, 2014-15
- Kombe la dunia kwa vlabu (3): 2009, 2011, 2015
- Taji la Super Cup barani Ulaya (3): 2009, 2011, 2015
- Ligi kuu ya soka nchini Uhispania (7): 2004-05, 2005-06, 2008-09, 2009-10, 2010-11, 2012-13, 2014-15
Orodha ya wachezaji waliowahi kunyakua taji la mchezaji bora duniani.
1956: Stanley Matthews (ENG) |
1957: Alfredo Di Stefano (ESP) |
1958: Raymond Kopa (FRA) |
1959: Alfredo Di Stefano (ESP) |
1960: Luis Suarez (ESP) |
1961: Omar Sivori (ITA) |
1962: Josef Masopust (CZE) |
1963: Lev Yachine (USSR) |
1964: Denis Law (SCO) |
1965: Eusebio (POR) |
1966: Bobby Charlton (ENG) |
1967: Florian Albert (HUN) |
1968: George Best (NIR) |
1969: Gianni Rivera (ITA) |
1970: Gerd Müller (GER) |
1971: Johan Cruyff (NED) |
1972: Franz Beckenbauer (GER) |
1973: Johan Cruyff (NED) |
1974: Johan Cruyff (NED) |
1975: Oleg Blokhine (URSS) |
1976: Franz Beckenbauer (GER) |
1977: Alan Simonsen (DEN) |
1978: Kevin Keegan (ENG) |
1979: Kevin Keegan (ENG) |
1980: Karl-Heinz Rummenigge (GER) |
1981: Karl-Heinz Rummenigge (GER) |
1982: Paolo Rossi (ITA) |
1983: Michel Platini (FRA) |
1984: Michel Platini (FRA) |
1985: Michel Platini (FRA) |
1986: Igor Belanov (USSR) |
1987: Ruud Gullit (NED) |
1988: Marco van Basten (NED) |
1989: Marco van Basten (NED) |
1990: Lothar Matthäus (GER) |
1991: Jean-Pierre Papin (FRA) |
1992: Marco van Basten (NED) |
1993: Roberto Baggio (ITA) |
1994: Hristo Stoïchkov (BUL) |
1995: George Weah (LBR) |
1996: Matthias Sammer (GER) |
1997: Ronaldo (BRA) |
1998: Zinédine Zidane (FRA) |
1999: Rivaldo (BRA) |
2000: Luis Figo (POR) |
2001: Michael Owen (ENG) |
2002: Ronaldo (BRA) |
2003: Pavel Nedved (CZE) |
2004: Andrei Shevchenko (UKR) |
2005: Ronaldinho (BRA) |
2006: Fabio Cannavaro (ITA) |
2007: Kaka (BRA) |
2008: Cristiano Ronaldo (POR) |
2009: Lionel Messi (ARG) |
2010: Lionel Messi (ARG) |
2011: Lionel Messi (ARG) |
2012: Lionel Messi (ARG) |
2013: Cristiano Ronaldo (POR) |
2014: Cristiano Ronaldo (POR) |
2015: Lionel Messi (ARG) |