Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli anafahamika kwa usemo wa hapa kazi tu, na wengine wanamwita Mzee wa kutumbua majipu kutokana na jitihada zake za kupambana na ufisadi na kuhakikisha kuwa taifa hilo linakuwa na watu wanaofanya kazi kwa bidii.
Huu ni usemi mwafaka, kwa rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa aliyechaguliwa siku ya Jumatano jijini Nairobi.
Kumekuwa na madai ya kufujwa kwa fedha kutoka FIFA za kuendeleza soka na pia zile kutoka serikalini, wachezaji wa timu ya taifa kutolipwa kwa wakati lakini pia kufutwa kazi kwa makocha wa timu ya taifa.
Mwendwa kwa kupata kura 50 katika uchaguzi huo na kumshinda Mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia Ambarose Rachier, inaonesha imani na kiu waliyonao Wakenya kutaka mabadiliko katika mchezo wa soka.
Kenya imekuwa ikishindwa kuendeleza soka la vijana na kuisababishia Harambee Stars katika mechi mbalimbali za Kimataifa.
Rais huyo mypa mwenye umri wa miaka 37, aliongoza vuguvugu lililotaka mabadiliko “Team Change” na ndio kitu ambacho wapenzi wa soka nchini Kenya wanataka kukiona.
Kazi ni kwa Nick Mwendwa ambaye sasa anahitaji ushirikiano wa wadau wote wa soka.
Huu ni mwamko mpya wa soka soka nchini Kenya.
Viongozi waliowahi kuongoza soka nchini Kenya:-
1963-1964 Isaac Lugonzo
1964-1968 John Kasyoka
1968–1970Kamati maalum ikiongozwa Jonathan Njenga
1970-1973 Martin Shikuku
1973 Kamati maalum ikiongozwa Billy Martin
1973-1974 William Humphrey Ngaah
1974-1975 Dan Owino
1975-1978 Kenneth Matiba
1978-1980 Dan Owino
1980–1984 Clement Gachanja
1984-1992 Job Omino
1992-1996 Kamati maalum ikiongozwa Matthew Adams Karauri
1996-2000 Peter Kenneth
2001-2004 Maina Kariuki
2004 Kamati maalum ikiongozwa Kipchoge Keino
2004-2007 Alfred Sambu
2007–2011 Mohamed Hatimy
2011–2015 Sam Nyamweya
2016- Nick Mwendwa